KATIBA YA KENYA,2010
Updated: Jul 7, 2021
UTANGULIZI SURA YA KWANZA - UKAMILIFU WA UKUU WA JUMUIA NA MAMLAKA YA KATIBA HII 5 1. UKAMILIFU WA UKUU WA NGUVU ZA JUMUIA 2. MAMLAKA YA KATIBA 3. ULINZI WA KATIBA
SURA YA PILI - JAMHURI 4. IKIRARI YA JAMHURI 5. ENEO LA KENYA 6. UGATUZI NA UPATIKANAJI WA HUDUMA 7. LUGHA NA NJIA ZA MAWASILIANO 8. NCHI NA DINI 9. NEMBO NA SIKU ZA KITAIFA. 10. THAMANI ZA KITAIFA NA KANUNI ZA UTAWALA. 11. UTAMADUNI
SURA YA TATU – URAIA. 12. ENTITLEMENTS OF CITIZENS 13. KUDUMISHA NA KUPATA URAIA 14. URAIA KWA KUZALIWA 15. URAIA KWA KUJIANDIKISHA 16. URAIA MARA KADHAA 17. KUBATILISHWA KWA URAIA 18. LEGISLATION ON CITIZENSHIP
SURA YA NNE – SHERIA YA HAKI SEHEMU YA KWANZA- VIPENGELE VYA JUMLA KUHUSIANA NA SHERIA YA HAKI 19. HAKI NA HURU ZA KIMSINGI 20. UTEKELEZAJI WA SHERIA YA HAKI 21. UTEKELEZAJI WA HAKI NA HURU ZA KIMSINGI 22. UTEKELEZAJI WA SHERIA YA HAKI 23. MAMLAKA YA MAHAKAMA KUDUMISHA NA KUTEKELEZA SHERIA YA HAKI 24. MIPAKA YA HAKI NA HURU ZA KIMSINGI 25. HAKI NA HURU MSINGI AMBAZO HAZIWEZI KATIZWA (KUWA LIMITED)
SEHEMU YA PILI – HAKI NA HURU ZA KIMSINGI 26. HAKI YA UHAI 27. USAWA NA HURU KUTOKA (DHIDI YA) UBAGUZI 28. HADHI YA KIBINADAMU.. 29. UHURU NA USALAMA WA MTU. 30. UTUMWA NA KAZI YA KULAZIMISHWA. 31. PRIVACY – USIRI?. 32. UHURU WA DHAMIRI, DINI, IMANI NA MAONI 33. UHURU WA KUJIELEZA.. 34. UHURU WA VYOMBO VYA HABARI 35. UWEZO WA KUAFIKIA HABARI (ACCESS TO INFORMATION). 36. UHURU WA KUTANGAMANA.. 37. MIKUTANO, MAANDAMANO, MIGOMO NA MALALAMISHI 38. HAKI ZA KISIASA.. 39. UHURU WA KUTEMBEA (MOVEMENT) NA KUISHI (RESIDENCE) 40. ULINZI WA HAKI YA KUMILIKI MALI 41. MAHUSIANO YA KIKAZI 42. MAZINGIRA 43. HAKI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII 44. LUGHA NA UTAMADUNI 45. FAMILIA. 46. HAKI ZA WATUMIAJI (CONSUMERS) 47. HATUA YA HAKI YA KIUTAWALA (FAIR ADMINISTRATIVE ACTION) 48. UWEZO WA KUPATA HAKI 49. HAKI ZA WALIOKAMATWA (ARRESTED PERSONS) 50. HAKI KATIKA KUSIKIZWA KWA KESI 51. HAKI ZA WALIO VIZUIZINI (DETAINED, HELD IN CUSTODY OR IMPRISONED)
SEHEMU YA TATU- UTUMIZI MAALUM WA HAKI 52. TAFSIRI YA SEHEMU.. 53. WATOTO.. 54. WALEMAVU.. 55. VIJANA.. 56. MAKUNDI MADOGO NA MAKUNDI TENGWA.. 57. WAZEE KATIKA JAMII 58. HALI YA HATARI 59. TUME YA HAKI NA USAWA.. KATIBA YA KENYA UTANGULIZI Sisi, Jumuia ya Kenya[1] TUKITAMBUA utukufu wa Mungu Muumba wa vyote vilivyo TUKIWAHESHIMU mashujaa waliopigania uhuru na haki ya nchi yetu TUKIJIVUNIA wingi[2] wa kabila, tamaduni na dini zetu na kuazimia kuishi kwa amani na umoja tukiwa taifa moja dhabiti TUKITHAMINI mazingira yetu, ambayo ndiyo urithi wetu na kuazimia kuyadumisha kwa manufaa ya vizazi vijavyo: TUKIJITOLEA kukuza na kuhifadhi maslahi ya watu binafsi, familia, jamii na taifa TUKITAMBUA matarajio ya Wakenya wote kwa serikali iliyo na misingi bora ya haki za binadamu, usawa, uhuru, demokrasia, haki za kijamii na utawala wa sheria[3] TUKITUMIA haki zetu kuu na kamilifu[4] zisizoshindwa[5] za kujichagulia na kujiamulia aina ya uongozi wa nchi yetu na tukiwa tumeshiriki kikamilifu katika kuiunda katiba hii: TUNAIKUBALI[6], TWAIPITISHA[7] na kujipa katiba hii kwetu wenyewe na kwa vizazi vijazo. MUNGU AIBARIKI KENYA SURA YA KWANZA - UKAMILIFU WA UKUU WA JUMUIA NA MAMLAKA YA KATIBA HII
1. UKAMILIFU WA UKUU WA NGUVU ZA JUMUIA 1) Nguvu zote za kitawala zinamilikiwa na jumuiya ya[8] Kenya na hazitatumika[9] ila kulingana na Katiba hii. 2) Jumuia ya Kenya inaweza kutumia nguvu za uu za kitawala moja kwa moja au kupitia kwa wawakilishi waliochaguliwa kidemokrasia 3) Mamlaka chini ya hii Katiba yamepewa taasisi zifuatazo za Serikali, ambazo zitatekeleza majukumu yao kulingana na hii Katiba – a) Bunge za kitaifa na mabaraza ya kutunga sheria katika serikali zilizogatuliwa; b) Serikali ya kitaifa na miundo yake katika serikali zilizogatuliwa; c) Idara ya mahakama na mojopo mengine huru; 4) Mamlaka ya jumuia inatumika katika: a) Kiwango cha kitaifa b) Kiwango cha kaunti
2. MAMLAKA YA KATIBA (1) Katiba hii ndio sheria kuu ya Jamhuri na inaunganisha watu wote na taasisi zote za nchi katika viwango vyote vya kiserikali – (2) Hakuna mtu yeyote anayeweza kudai au kutumia mamlaka ya Nchi bila idhini au kulingana na jinsi ilivyoidhinishwa na Katiba hii. (3) Uhalali[10] na utekelezaji[11] wa katiba hii hauwezi kupingwa na au katika mahakama yoyote au tawi lolote la Serikali. (4) Sheria yoyote, ikiwemo sheria ya mila na tamaduni, ambayo haiambatani na Katiba hii haitambuliwi kwa kiasi hicho ambacho haiambatani, na kitendo chochote ama kutotimiza wajibu kinyume na Katiba hii si halali. (5) Sheria za kijumla za mataifa zitakuwa sehemu ya sharia za Kenya (6) Mkataba au mapatano[12] ambayo imekubaliwa na Kenya itazingatiwa kama sharia ya Kenya kulingana na Katiba hii.
3. ULINZI WA KATIBA (1) Kila mtu ana jukumu la kuiheshimu , kuitetea na kuilinda katiba hii. (2) Jaribio lolote la kubuni serikali vingineila kulingana na Katiba hii ni haramu.
SURA YA PILI - JAMHURI
4. IKIRARI YA JAMHURI (1) Kenya ni Nchi Huru (2) Jamhuri ya Kenya ni demokrasia na siasa za vyama vingi ambayo imejikita kwenye misingi ya maadili za kitaifa na kanuni za utawala bora ambazo zimenakiliwa katika Kifungu cha 10.
5. ENEO LA KENYA Kenya inajumuisha eneo la maji na nchi kavu zinazojumuisha Kenya on the effective date, na maeneo mangine ya nchi kavu au maji ambazo zimetambulishwa na Sheria za Bunge.
6. UGATUZI NA UPATIKANAJI[13] WA HUDUMA (1) Eneo la Kenya limejumuisha[14] Kaunti ambazo zimenakiliwa katika Awamu ya Kwanza. (2) Serikali katika kiwango cha Kitaifa na kiwango cha Kaunti ni tofauti ila zinategemeana na zitawasiliana kwa msingi ya mashauriano na ushirikiano.
7. LUGHA NA NJIA ZA MAWASILIANO. (1) Lugha ya taifa ni Kiswahili. (2) Lugha rasmi za Kenya ni Kiswahili na Kiingereza. (3) Serikali- a) Itakuza na kulinda wingi wa lugha wa watu wa Kenya b) itakuza maendeleo na matumizi ya lugha za kiasili, lugha ya ishara, breli na njia zingine za mawasiliano kwa watu wenye ulemavu. 8. NCHI NA DINI Hakutakuwa na dini ya Taifa.
9. NEMBO NA SIKU ZA KITAIFA (1) Nembo za kitaifa za Jamhuri ni – a) Bendera ya taifa; b) Wimbo wa taifa; c) Ngao ya ulinzi; na d) Muhuri wa serikali (2) Nembo za kitaifa zimenakiliwa katika ratiba ya pili (3) Siku kuu za kitaifa ni – a) Siku kuu ya Madaraka, kuadhimishwa Juni 1; b) Siku kuu ya Mashujaa, kuadhimishwa Oktoba 20; na c) Siku kuu ya Jamhuri, kuadhimishwa Desemba 12. (4) Siku ya kitaifa itakuwa ya mapumziko kote nchini. (5) Bunge linaweza, kupitia kwa sheria kuamua ni siku gani iwe ya kitaifa, na namna ya kusherehekea siku hiyo
10. THAMANI ZA KITAIFA NA KANUNI ZA UTAWALA (1) Thamani za kitaifa na kanuni za utawala katika yaliyomo katika Sura hii yatafuatwa na taasisi mbalimbali za Serikali, Maafisa wa Serikali na watu wote kila yeyote kati yao – a. anatekeleza au anafasiri Katiba hii; b. anatumia, anatekeleza au kufasiri sheria yoyote; au c. anafanya, anatumia au anatekeleza maamuzi kuhusu sera ya kitaifa (2) Thamani za kitaifa na kanuni za utawala ni pamoja na: a. Uzalendo, umoja wa kitaifa, ushirikiano[15] na ugatuzi wa mamlaka, Utawala wa sheria, demokrasia na ushiriki wa watu katika masuala ya kiserikali; b. Heshima na utu wa kibinadamu[16], usawa[17], haki ya kijamii, ujumuishaji, usawa[18], haki za kibinadamu, kutokuwa na ubaguzi na utetezi wa haki za waliotengwa na jamii; c. utawala bora, uadilifu, uwazi na uwajibikaji; na d. Maendeleo ambayo yanaweza kudumishwa.
11. UTAMADUNI (1) Katiba hii inatambua utamaduni kama msingi wa taifa na mkusanyo wa ustaarabu wa watu wa Kenya na taifa. (2) Serikali- a. Itakuza aina zote za kujieleza za kitaifa na za kitamaduni kupitia fasihi, sanaa, sherehe za kitamaduni, sayansi, mawasiliano, habari, vyombo vya habari, machapisho na maktaba na njia nyingine za kitamaduni; b. kutambua jukumu la sayansi na teknolojia za kiasili katika maendeleo ya nchi; na c. kupitia kwa sheria, kutambua na kulinda haki miliki za maarifa ya watu wa Kenya. (3) Bunge litaunda sheria — a. kuhakikisha kwamba jamii zinapewa fidia au mrabaha kwa kutumiwa kwa turathi zao za kitamaduni; na b. Kutambua na kulinda umiliki wa mbegu na mimea ya kiasili, sifa zao za kimaumbile na matumizi yao na jamii za Kenya.
SURA YA TATU – URAIA
12. ENTITLEMENTS OF CITIZENS (1) Kila raia anastahili – a) haki, mapendeleo na faida ya uraia kulingana na mipaka iliyowekwa na Katiba hii; na b) Pasipoti ya Kenya na stakabadhi yoyote ya usajili na utambulisho inayotolewa na Serikali kwa raia wake. (2) Pasipoti na stakabadhi nyingine ambazo zimetambuliwa na clause (1)(b) inaweza kataliwa, suspended au kupokonywa kwa kufuata Sheria za bunge ambayo satisfies the criteria referred to in Article 24.
13. KUDUMISHA NA KUPATA URAIA (1) Kila mtu ambaye alikuwa raia kabla ya tarehe ya utekelezaji anadumisha uraia wake kuanzia tarehe hiyo. (2) Uraia unaweza kupatikana kwa kuzaliwa, au kujisajili. (3) Uraia haupotezwi kupitia kwa ndoa au kuvunjika kwa ndoa
14. URAIA KWA KUZALIWA (1) Mtu ni raia wa kuzaliwa iwapo wakati wa tarehe ya kuzaliwa kwa mtu huyo, ama mama au baba yake ni raia. (2) Clause (1) itatumika kwa mtu aliyezaliwa kabla ya the effective date, ikwiwa baba au mama yake alikuwa raia bila kuzangitia ikiwa lizaliwa Kenya au la. (3) Bunge inawezapitisha sheria kupunguza utumizi wa clauses (1) and (2) kwa vizazi vyaraia wa Kenya walizaliwa nje ya nchi. (4) Mtoto anayepatikana nchini Kenya ambaye ni, au anaonekana kuwa na umri wa miaka minane, na ambaye uraia wake na wazazi hawajulikani , anachukuliwa[19] kuwa raia kwa kuzaliwa. (5) Mtu ambaye ni raia wa Kenya, na kwa sababu ya kujipatia uraia wa nchi nyingine alikoma kuwa raia wa Kenya ana haki, kwa kutuma maombi, kurejeshewa uraia wa Kenya.
15. URAIA KWA KUJIANDIKISHA (1) Mtu ambaye ameolewa na raia kwa muda wa angalau miaka saba ana haki, kwa kutuma maombi, kuandikishwa kama raia. (2) . Mtu ambaye amekuwa mkazi halali nchini Kenya kwa muda wa miaka saba mfululizo, na ambaye anatimiza masharti yote ya sheria yaliyoidhinishwa na Bunge, anaweza kutuma maombi ya kujiandikisha kama raia. (3) ) Mtoto ambaye sio raia na ambaye ni wa kupanga na raia ana haki, kwa kutuma maombi, kuandikishwa kama raia. (4) . Bunge litaunda sheria kueleza taratibu kupitia kwazo uraia (wa Kenya) unaweza kupewa raia wa nchi zingine. (5) This Article itatumika kwa mtu kutoka the effective date, lakini matakwa yoyote ambazo lazima yatimizwe kabla mtu kuwa na entitlement ya kuandikishwa kama rais yatazingatiwa kutimizwa bila kujali ikiwa yalitimizwa kabla ya au baada ya the effective date, au sehemu nyingine ilitimizwa kabla na sehemu nyingine ikatimizwa baada ya the effective date.
16. URAIA MARA KADHAA[20] (1) Mtu ambaye ni raia hapotezi uraia wake kwa sababu ya kujipatia uraia wa nchi nyingine
17. KUBATILISHWA KWA URAIA (1) Ikiwa mtu alipata uraia wake kupitia kuandikishwa, uraia wake unaweza batilishwa ikiwa – a) Mtu huyo alipata uraia huo kupitia ulaghai, udanganyifu, na kufichwa kwa any material fact; b) Mtu huyo, wakati Kenya imeshiriki vita, alishiriki biashara kiharamu au aliwasiliana na adui au alishiriki au kujihusisha na biashara ambayo ilifanywa na maarifa kwamba itamsaidia adui katika vita hizo; c) Mtu huyo, ndani ya miaka mitano baada ya kuandikishwa, amehukumiwa kwa kosa na kupewa kifungo cha miaka tatu au Zaidi; au d) Mtu huyo, wakati wowote baada ya kuandikishwa, amehukumiwa uhaini, au kwa kosa ambayo – i. Hukumu ya angalau miaka saba inaweza pitishwa; au ii. Hukumu nyingine kali Zaidi inaweza pitishwa Uraia wa mtu ambaye alipata uraia wake kupitia kudhaniwa kuwa raia wa kuzaliwa, kulingana na Article 14 (4), unaweza batilishwa ikiwa- a) Uraia ulipatikana huo kupitia ulaghai, udanganyifu, na kufichwa kwa any material fact; b) Uraia au uzazi wa mtu huyo umejulikana, na imepatikana kwamba mtu huyo ni raia wan chi nyingine; au c) Umri wa mtu huyo imejulikana, na ikapatikana kwamba alikuwa Zaidi ya miaka nane alipopatikana Kenya.
18. SHERIA YA URAIA (LEGISLATION ON CITIZENSHIP) Bunge itapitisha sheria- a) Ikiigiza utaratibu ambazo zinaweza tumika kwa mtu kuwa raia; b) Kudhibitisha kuingia au kupata makaazi Kenya c) providing for the status of permanent residents d) kutoa nafasi kwa kukataa uraia kwa kupenda; e) kueleza taratibu kupitia kwazo uraia unaweza batilishwa; f) kueleza majukumu na haki za Raia; na g) Kwa jumla , kutoa athari kwa vipengele vya Sura hii SURA YA NNE – SHERIA YA HAKI SEHEMU YA KWANZA- VIPENGELE VYA JUMLA KUHUSIANA NA SHERIA YA HAKI
19. HAKI NA HURU ZA KIMSINGI (1) Sheria hii ya Haki ni kiungo muhimu katika utawala wa kidemokrasia nchini Kenya na ndiyo msingi wa sera za kijamii, kiuchumi na kitamaduni. (2) Umuhimu wa kutambua na kulinda haki za kibinadamu na uhuru muhimu ni kulinda heshima ya watu binafsi na jamaa na kukuza haki za kijamii na utambuaji wa uwezo wa binadamu wote. (3) Haki na uhuru wa kimsingi zinazotajwa katika sura hii- (a) ni za kila mtu binafsi na wala hazitolewi na serikali; (b) hazitengi haki na uhuru mwingine wa kimsingi ambao haukutajwa katika Sura hii, lakini zinazotambuliwa na kukubaliwa na sheria, ila endapo ni kwa kiwango ambapo hazikubaliani na sura hii; na (c) Hazitazingatia mipaka yoyote ila mipaka inayoelezwa katika Katiba hii. 20. UTEKELEZAJI WA SHERIA YA HAKI (1) Sheria ya Haki inahusu sheria zote na inajumlisha mashirika yote ya Serikali na watu wote. (2) Kila mtu atafurahia haki na uhuru wa kimsingi uliotajwa katika Sheria ya Haki, kwa kiwango kikubwa kuambatana na hali ya haki au uhuru wa kimsingi. (3) Katika kutekeleza kipengele Sheria ya Haki, mahakama inapaswa a) kutekeleza sheria kwa kiwango ambacho hakiathiri haki au uhuru wowote wa kimsingi; na b) Kuegemea fasiri inaendana na utekelezaji wa haki au uhuru wa wa kimsingi. (4) Katika kufasiri Sheria ya Haki, mahakama, mahakama maalumu, au mamlaka nyingine zitakuza a) maadili yanayoongoza jamii huru na ya kidemokrasia kulingana na heshima ya ubinadamu, ulinganifu, usawa, na uhuru; na b) imani, madhumuni na kusudi la Sheria ya Haki. (5) Wakati wa utekelezaji wa haki yoyote chini ya Kifungu 43, endapo serikali inadai kuwa haina raslimali za kutekeleza haki hiyo, Shirika la kiserikali,mahakama, mahakama maalumu, au mamlaka nyingine yoyote itaongozwa na kanuni zifuatazo – a) ni jukumu la serikali kuonyesha kuwa raslimali hazipo; b) katika kugawa raslimali, serikali ina jukumu la kuipa kipaumbele uhakikishaji wa uwezekano mkubwa wa kufurahia haki au uhuru wa kimsingi kwa kuzingatia hali halisi, ikiwemo kutengwa kwa baadhi ya makundi au watu binafsi; na c) Mahakama, mahakama maalumu, Tume ya Haki za Kibinadamu na Maswala ya Kijinsia au mamlaka nyingine haipaswi kuingilia uamuzi wa Asasi ya serikali kuhusu ugavi wa raslimali zilizopo, hasa kwa misingi kuwa utakuwa umefikia uamuzi tofauti.
21. UTEKELEZAJI WA HAKI NA HURU ZA KIMSINGI (1) Ni jukumu la kimsingi la serikali na kila Asasi ya serikali kuzingatia, kuheshimu, kulinda, kukuza na kuhakikisha haki na uhuru wa kimsingi katika Sura hii, ilivyokatika utumizi wa nguvu na majukumu yao. (2) Serikali itachukua hatua za kisheria, kisera na nyinginezo kuafiki utambuaji wa haki zinazotolewa chini ya kifungu 43 (3) Mashirika yote ya serikali na maofisa wa serikali wana jukumu la kuelewa, kujitahidi wenyewe kukabiliana na mahitaji ya makundi maalumu katika jamii, wakiwemo wanawake, wazee, walemavu, watoto, vijana na makundi yaliyotengwa, jumuia tengwa na wa jumuia fulani za kikabila, kidini na kitamaduni. (4) Serikali itasambaza kwa umma Maoni na Mapendekezo ya Jumla ya mashirika ya kimataifa ya haki za kibinadamu kuhusiana na utekelezaji wa malengo yake ya kimataifa
22. UTEKELEZAJI WA SHERIA YA HAKI (1) Kila mtu ana haki ya kuanzisha kesi mbele ya mahakama , kudai kuwa haki au uhuru wa kimsingi uliodokezwa katika Sheria ya Haki havijazinga tiwa,zimekiukwa, zimevunjwa au zimetishiwa – (2) Pamoja na mtu kujitetea, malalamishi mbele ya mahakama kulingana na Clause 1 inaweza anzishwa na - a) mtu anayemwakilisha mtu mwingine asiyeweza kujiwakilisha; b) mtu mwanachama wa, au kwa hiari ya kundi au tabaka fulani la watu; c) mtu aliyejitolea kwa niaba ya umma; na d) muungano uliojitolea kwa niaba ya mmoja au kundi miongoni mwa wanachama. (3) Jaji Mkuu ataweka kanuni zinazoruhusu kesi zilizotajwa katika Article hii, ambazo zitazingatia vigezo kwamba– a) haki za kulalamika zilizotolewa katika Kifungu (2) zinatekelezwa kwa ukamilifu; b) Urasmi unaohusiana na kesi hizo , ikiwemo kuanzishwa kwa kesi, unawekwa kwa kiwango cha chini, na hasa kwamba pakiwa na haja, mahakama itakubali kuwepo wa kesi kwa misingi ya rekodi zisizo na lazima ya urasmi; c) Hakuna fedha zitakazotozwa kwa kuanzisha kesi chini ya Kifungu hiki; d) Mahakama, kwa kuzingatia kanuni za haki za kimsingi haitazuiwa bila sababu na mahitaji madogo madogo; na e) Shirika au mtu binafsi mwenye ujuzi maalumu anaweza kwa idhini ya mahakama, kujitokeza kama rafiki ya mahakama (4) Kukosekana kwa kanuni zinazoangaziwa katika Clause (3) hakutamnyima yeyote haki ya kuanzisha lalama chini ya Katiba hii na kusikizwa kwa lalama hiyo na kushughulikiwa na mahakama.
23. MAMLAKA YA MAHAKAMA KUDUMISHA NA KUTEKELEZA SHERIA YA HAKI (1) Mahakama Kuu ina mamlaka kwa mujibu wa Article 165 kusikiliza na kuamua maombi dhidi ya kunyimwa, ukiukaji, na tishio dhidi ya haki za kibinadamu au huru za kimsingi uliotajwa katika Sheria ya Haki. (2) Bunge litatunga sheria kutoa uwezo wa kiasili kwa mahakama za chini katika kusikiza maombi ya kusikizwa upya kwa ukiukaji wa Sheria ya Haki. (3) ) Katika kesi yoyote inayoletwa mbele yake chini ya Article 22, mahakama inaweza kutoa usaidizi, ikiwemo- a) kukiri haki; b) agizo la mahakama; c) amri ya uhifadhi; d) utangazaji kutotakikana tena kwa sheria yoyote inayotatiza Sheria ya Haki na haikubaliwi kwa misingi ya Article 24; e) amri ya kufidiwa dhidi ya Serikali au mtu yeyote anayehusika na uvunjaji wa haki au uhuru wowote wa kimsingi; na f) amri ya marekebisho ya kisheria
24. MIPAKA YA HAKI NA HURU ZA KIMSINGI (1) Haki na huru zilizonakiliwa katika Bill of Rights hazitawekwa mipaka isipokuwa kupitia sharia, na hata hivyo mipaka hiyo itawekwa kufuatia migezo ya kuwa reasonable na justifiable katika demokrasia huru ambayo ni based on human dignity, usawa na uhuru, ikizingatia mambo husika ikiwemo: a) Hali ya haki hiyo au uhuru huo wa kimsingi b) Umuhimu wa jukumu la mpaka huo c) Hali na kiwango cha mipaka hiyo d) Haja ya kuhakikisha kuwa ufurahiaji wa haki hizo na uhuru huo wa kibinafsi na mtu yeyote hautatizi haki na uhuru wa kimsingi wa wengine; na e) Uhusiano uliopo kati ya mpaka na jukumu lake na endapo kuna njia nyingine zisizotatiza sana kuafikia jukumu hilo. (2) Licha ya Clause (1), , kifungu cha kisheria kinachowekea mipaka haki au uhuru wa kimsingi- a) Haikubaliki katika sheria iliyotungwa au kurekebishwa baada ya siku ya kutekeleza katiba hii, isipokuwa sheria hiyo ikidhihirisha nia ya kuzuia haki hiyo au uhuru huo na hali na kiwango cha mipaka hiyo; b) haitachukuliwa kama uzuiaji haki au uhuru uliotajwa katika Sheria ya Haki isipokuwa pale ambapo kipengele cha sheria kinaeleza wazi na kwa yakini kuhusu haki au uhuru wa kimsingi unaopaswa kuzuiwa na hali au kiwango cha mipaka hiyo; na c) Haitazuia haki au uhuru wa kimsingi unaotajwa katika Sheria ya Haki ili kupuuza maswala nyeti na muhimu katika haki hiyo. (3) Serikali au mtu anayetaka kutosheleza a particular limitation atapaswa kuthibitishia mahakama, mahakama maalumu au mamlaka nyingine kuwa mahitaji ya Kifungu hiki yamezingatiwa. (4) Maelezo ya Sura hii kuhusu usawa yatakubaliwa hadi kwa viwango vya utekelezaji wa Sharia ya Kiislamu kwa waumini wa Kiislamu kwa mujibu wa hadhi zao za kibinafsi, hali ya ndoa, talaka na urithi. (5) Licha ya Clause (1) na (2), kifungu cha sharia inaweza weka mipaka limiting the application ya haki na huru za kimsingi katika vifungu kwa watu ambao wanahudumu kwenye Kenya Dfence Forces au The National Police Service – a) Article 31—Privacy; b) Article 36— Uhuru wa kushirikiana; c) Article 37—Mkutano, Maandamano, picketing and petition; d) Article 41—Mahusiano ya kikazi; e) Article 43—Haki za kiuchumi na kijamii; na f) Article 49— Haki ya watu waliokamatwa 25. HAKI NA HURU MSINGI AMBAZO HAZIWEZI KATIZWA (KUWA LIMITED) Licha ya chochote katika Katiba hii, hakutakuwa na uwekaji mipaka kwa haki na huru za kimsingi zifuatazo - a) Uhuru dhidi ya mateso na ukatili, unyanyasaji au adhabu za kinyama zinazokiuka ubinadamu; b) Uhuru dhidi ya utumwa; c) Haki ya fair trial ; na d) Haki ya kuitikiwa amri ya kufikishwa mahakamani
SEHEMU YA PILI – HAKI NA HURU ZA KIMSINGI
26. HAKI YA UHAI
(1) Kila mtu ana haki ya uhai[21]
(2) Uhai wa mtu utaanza akiwa mimba (at conception)
(3) Mtu yeyote hatanyngánywa uhai wake kimakusudi, ila kwa kuzingatia the extent ambayo imeidhinishwa na katiba hii au sharia nyingine ilioandikwa (written law)
(4) Kuavya mimba haijaidhinishwa isipokuwa katika maoni ya trained health professional, kuna haja ya emergency treatment, au uhai au afya ya mama imo hatarini, au imekubalika na sharia nyingine (written law)
27. USAWA NA HURU KUTOKA (DHIDI YA) UBAGUZI
(1) Kila mtu ni sawa mbele ya sheria na ana haki ya kulindwa na manufaa sawa ya sharia
(2) Usawa unajumuisha ufurahiaji kwa ukamilifu haki zote na uhuru wote wa kimsingi.
(3) Wanawake na wanaume wana haki ya kushughulikiwa kwa usawa ikiwemo haki ya kupata nafasi sawa katika shughuli za kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na kijamii.
(4) Serikali haitabagua kwa vyovyote dhidi ya mtu yeyote kwa misingi yoyote ikiwemo asili, jinsia, mimba, hadhi ya kindoa, hali ya kiafya, asili ya kikabila au kijamii, rangi, umri, ulemavu, dini, dhamiri, imani, utamaduni, mavazi, lugha au kuzaliwa.
(5) Mtu hatambagua mwingine kwa vyovyote dhidi ya mwingine kwa misingi imetambulishwa au yametafakariwa Clause 4.
(6) Serikali itachukua hatua za kisheria na nyinginezo, ikiwemo japo sio lazima mipango ya usawa na sera zilizopangwa kushughulikia upya matatizo yaliyomkumba mtu yeyote au makundi kwa mujibu wa ubaguzi wa mbeleni
(7) Hatua yoyote inayochukuliwa chini ya Clause (6) itatoa nafasi kwa manufaa kuwa misingi ya haja maalumu.
(8) Pamoja na the measures contemplated in Clause 6, serikali itachukuwa mikakati ya kisheria na mengineyo to implement the principle that not more than two-thirds of the members of elective or appointive bodies shall be of the same gender.
28. HADHI YA KIBINADAMU
Kila mtu ana hadhi ya kiasili na haki ya kuheshimiwa na kulindwa kwa hadhi hiyo
29. UHURU NA USALAMA WA MTU
Kila mtu ana haki ya uhuru na usalama wake, unaojumuisha haki dhidi ya –
(a) Kunyimwa uhuru kiholela au bila sababu mwafaka;
(b) Kufungwa bila kushtakiwa mahakamani, isipokuwa wakati wa hali ya hatari ambapo kifungo cha sampuli hiyo kinaelezwa katika Article 58
(c) Aina zote za ghasia kutoka kwa umma au watu binafsi;
(d) Kuteswa katika njia yoyote ile, iwe ya kimwili au kisaikolojia;
(e) Adhabu ya viboko
(f) Kuteswa au Kupewa adhabu kali, kudhalilishwa au kushughulikiwa Kinyama.
30. UTUMWA NA KAZI YA KULAZIMISHWA
(a) Hakuna mtu atayewekwa katika utumwa.
(b) Mtu hatahitajika kufanya kazi ya kulazimishwa.
31. PRIVACY – USIRI?
Kila mtu anayo haki ya usiri wake, inayojumuisha haki ya–
(a) kutosakwa kwao , nyumba au maboma yao wala mali yao;
(b) milki yao kusanywa au kunyakuliwa;
(c) Habari kuhusiana na familia zao au mambo yao siri kuulizwa au kufichuliwa kiholela; au
(d) siri za mawasiliano yao kuvunjwa
32. UHURU WA DHAMIRI, DINI, IMANI NA MAONI
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kuwa na msimamo, dini, mawazo, imani na maoni –
(2) Kila mtu anayo haki, ama kibinafsi au na wengine katika jumuia, kwa wazi au kisiri, kufuata dini au imani yoyote kupitia ibada, matendo, mafunzo, au maadhimisho ikiwemo mazingatio ya siku za ibada.
(3) Mtu hapaswi kuzuiwa kuafikia taasisi yoyote, ajira au jengo au kufurahia haki yoyote kwa sababu ya imani zao za kidini.
(4) Mtu hatalazimishwa kushiriki katika kitndo chochote kisichoambatana na imani au dini ya mtu huyo.
33. UHURU WA KUJIELEZA
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kujieleza unaojumuisha –
a. uhuru wa kutafuta, kupokea au kutoa habari au kauli;
b. uhuru wa kubuni kisanii; na (c) uhuru wa kiakademia na utafiti wa kisayansi.
(2) Haki ya kujieleza sio uhuru wa/ haifiki kwenye kiwango cha-
a. propaganda ya vita;
b. uchochezi wa ghasia
c. hotuba za chuki; au
d. utetezi wa chuki ambao-
i. unajumuisha uchochezi wa kikabila, matusi ya wengine au uchochezi wa kusababisha maafa; au
ii. unaotokana na misingi ya ubaguzi iliokataliwa kwa mujibu wa Article 27 (4)
(3) Katika kutumia uhuru wa kujieleza, kila mtu ataheshimu haki na sifa/hadhi ya wengine
34. UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
(1) Uhuru na kujitegemea kwa vyombo vya matangazo, kuchapisha na vingine vya habari vya aina yoyote unahakikishwa, ila uhuru huo haujaunga kujieleza kwowote kinyume na Article 33(2).
(2) Serikali –
(a) haitasimamia au kuingilia mtu yeyote anayehusika na utangazaji, uchapishaji au usambazaji wa chapisho lolote au usambazaji wa habari kwa kutumia chombo chochote; au
(b) Haitamwadhibu mtu yeyote kwa maoni au mawazo au maswala ya utangazaji, uchapishaji au usambazaji.
(3) Vyombo vya utangazaji na vyombo vingine vya habari vina uhuru wa kuanzisha chochote, isipokuwa kwa kuongozwa na taratibu za leseni ambazo-
(a) zimeratibiwa kuhakikisha udhibiti wa mawimbi ya hewa na aina nyingine usambazaji wa mawimbi; na
(b) Haziingiliwi na serikali, hisia za kisiasa au za kibiashara.
(4) Vyombo vyote vya habari vianvyomilikiwa na serikali-
(a) Vitakuwa huru kuweka makala ya kibinafsi ya kitahariri ya matangazo yao au mawasiliano mengine;
(b) Havitaegemea upande wowote; na
(c) Vitakuwa na nafasi ya kuwasilisha maoni tofauti tofauti na mawazo yanayokinzana.
(5) Bunge litatunga sheria itakayotoa nafasi ya kuanzisha shirika ambalo-
(a) Litakuwa huru dhidi ya serikali au mwingilio wa kisiasa;
(b) Litamulika maslahi ya sehemu zote za jamii; na
(c) Litaweka viwango na kudhibiti na kuchunguza uzingatiaji wa viwango hivyo
35. UWEZO WA KUAFIKIA HABARI (ACCESS TO INFORMATION).
(1) Kila mwananchi anayo haki ya kuafikia-
(a) Habari ilizonazo na Serikali; na
(b) Habari zozote zilizo na mtu mwingine na zinazohitajika ili kutekeleza au kulinda haki yoyote au uhuru wowote wa kimsingi.
(2) Kila mtu anayo haki ya kutaka kurekebishwa au kubatilishwa kwa habari zozote za uongo au za kupotosha zinazomhusu mtu huyo.
(3) Serikali itachapisha na kutangaza habari muhimmu inayohusu taifa
36. UHURU WA KUTANGAMANA
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutangamana, ambayo inaunganisha haki ya kutunga, kujiunga na, kushiriki shughuli za mashirika ya kila aina.
(2) Mtu hatalazimishwa kujiunga na muungano wa aina yoyote
(3) Sheria yoyote inayohitaji usajili wa miungano ya mashirika ya aina yoyote itahitaji kwamba-
(a) Usajili huo hauwezi kuzuiwa au kunyang’anywa bila sababu maalumu, na
(b) Kutakuwa na haki ya rufaa ya haki kabla ya usajili kukataliwa/kunyanganywa.
37. MIKUTANO, MAANDAMANO, MIGOMO NA MALALAMISHI
Kila mtu ana haki, kwa Amani na akiwa bila silaha, ya kukutana, kuandamana, kugoma, na kuwasilisha malalamishi yake kwa mamlaka ya umma.
38. HAKI ZA KISIASA
(1) Kila raia yuko huru ya kujifanyia uchangusi wa kisiasa. Ikiwemo haki ya-
(a) Kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa
(b) Kushiriki katika shughuli za, au kusajili wanachama kwa niaba ya chama; na
(c) Kufanya kampeni za chama cha kisiasa.
(2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki uchaguzi huru, wa haki na wa kila mara, ambapo kila mtu mzima ana haki ya kuchagua, na kila mchaguzi ako huru kueleza matakwa yake kuhusu –
(a) Shirika au ofisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya uchaguzi;
(b) Ofisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni mwanachama.
(3) Kila mtu mzima ana haki, bila vizuizi visivyo na sababu, ya-
(a) Kusajiliwa kama mpigakura
(b) Kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au referendum, na
(c) Kugombea wadhifa katika ofisi ya umma, au ofisi katika chama cha kisiasa ambacho wao ni wanachama na endapo atachaguliwa atashika usukani.
39. UHURU WA KUTEMBEA (MOVEMENT) NA KUISHI (RESIDENCE)
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutembea.
(2) Kila mtu ana haki ya kutoka nchini Kenya.
(3) Mwananchi ana haki ya kuingia, kubaki na kuishi kokote nchini Kenya.
40. ULINZI WA HAKI YA KUMILIKI MALI
(1) Isipokuwa kwa Article 65,kila mtu ana haki, ama kivyake au kwa ushirika na wengine, kupata na kumiliki mali
(a) Ya aina yoyote; na
(b) katika sehemu yoyote ya Kenya.
(2) Bunge halitatunga sheria inayoruhusu Serikali au mtu yeyote –
(a) Kumnyang’anya kiholela mtu yeyote mali ya aina yoyoye, au interest in, au haki kuhusu mali ya aina yoyote bila sababu maalum; au
(b) kuwekea mipaka au kuzuia kwa njia yoyote ufurahiaji wa haki yoyote chini ya Kifungu hiki kwa msingi wowote uliodokezwa katika Article 27 (4)
(3) Serikali haitamnyang’anya mtu yeyote mali ya aina yoyote, au interest in, au haki ya kuwa na mali ya aina yoyote isipokuwa endapo kunyang’anywa huko –
(a) unatokana na upataji wa ardhi au interest kwenye ardhi au conversion ya interest kwenye ardhi, au title kumiliki ardhi kwa mujibu wa Chapter 5; au
(b) ni kwa matumizi ya umma au ni kwa manufaa ya umma na inatekelezwa kwa mujibu wa Katiba hii au Sheria ya Bunge-
(i) Inayotaka malipo kwa ukamilifu ya kumfidia mtu huyo; na
(ii) Inayomruhusu mtu yeyote aliye na interest au haki juu ya mali hiyo uwezo wa kuafikia mahakama ya kisheria
(4) Kipengele kinaweza kuundwa ili kuwafidia wakaazi in good faith wa ardhi ambao huenda hawana umiliki ardhi hiyo.
(5) Serikali itaunga mkono,kukuza na kulinda haki miliki za maarifa ya watu wa Kenya
(6) Haki zilizonakiliwa chini ya Article hii haijaunga haki juu ya mali ambayo imepatikana kwamba ilipatikana kiharamu.
41. MAHUSIANO YA KIKAZI
(1) Kila mtu ana haki ya fair labour practices
(2) Kila mfanyakazi ana haki ya-
(a) kulipwa ipasavyo;
(b) masharti ya kufaa ya utendakazi;
(c) kuunda, kujiunga au kushirki katika shughuli na mipango ya vyama vya wafanyakazi; na
(d) kugoma
(3) ) Kila mwajiri ana haki ya-
(a) kuunda au kujiunga na miungano ya waajiri; na
(b) kushiriki katika shughuli na mipango ya miungano ya waajiri
(4) Kila chama cha wafanyakazi na miungano ya waajiri ina haki ya-
(a) kuamua usimamizi wake, mipango na shughuli zake;
(b) to organise;
(c) Kuunda na kujiunga na shirikisho.
(5) Kila chama cha wafanyakazi, muungano wa waajiri na mwajiri wana haki ya kushiriki katika maafikiano ya pamoja
42. MAZINGIRA
Kila mtu ana haki ya mazingira safi na salama (healthy?) ambayo inashirikisha haki ya
(a) Mazingira kutunzwa kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo kupitia hatua za kisheria na nyinginezo; na
(b) Kutekelezwa kwa majukumu inayohusiana na mazingira chni ya Article 70
43. HAKI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII
(1) Kila mtu ana haki –
(a) Kwa kiwango cha juu kabisa cha afya kinachowezekkana, ambayo ni pamoja na haki ya kupata huduma za afya ambazo ni pamoja na huduma ya afya ya uzazi
(b) . Kila mtu ana haki ya kufikia nyumba bora (accessible and adequate housing) na kwa viwango vya kufaa vya usafi
(c) Kila mtu ana haki ya kuwa huru dhidi ya njaa na kupata chakula cha kutosha kwa ubora wa kukubalika
(d) . Kila mtu ana haki ya kupata maji safi na salama katika viwango vya kutosha.
(e) Usalama wa kijamii
(f) Kupata elimu
(2) Hakuna mtu anayeweza kuzuiwa kupata matibabu ya dharura
(3) Serikali itatoa usalama wa kutosha wa kijamii kwa watu wasioweza kujisaidia au wanaoategemea.
44. LUGHA NA UTAMADUNI
(1) Kila mtu ana haki kutumia lugha na kushiriki katika maisha ya kitamaduni ya chaguo lake.
(2) Mtu anayetoka katika jumuia ya utamaduni au lugha fulani ana haki, pamoja na wanajumuia hiyo-
(a) Kufurahia utamaduni wake na kutumia lugha yake; au
(b) kuunda, kujiunga na kudumisha vyama vya kitamaduni na kilugha na miungano mingine ya raia katika jamii.
(3) Mtu hatamlazimisha mwingine kufanya, kuzingatia au kupitia kaida zozote za kitamaduni.
45. FAMILIA
(1) Familia ndio kitengo cha kiasili (natural) na kimsingi cha jamii na msingi muhimu katika mpangilio wa jamii, na itambuliwa na kulindwa na serikali.
(2) Kila mtu mzima anayo haki ya kuoa mtu wa jinsi tofauti kutokana na makubaliano yao.
(3) Wahusika katika ndoa wana haki sawa wakati wa kuoana, katika ndoa na wakati wa kuvunjwa ndoa yao.
(4) Bunge litatunga sheria inayotambua-
(a) ndoa zilizotekelezwa chini ya utamaduni wowote, au mfumo wowote wa sheria za kidini, sheria za binafsi (system of personal law) au sheria ya familia; na
(b) Sheria ya kibinafsi au familia chini ya utamaduni wowote, au inayofuatwa na watu waumini wa dini fulani, kwa kiwango kwamba ndoa au mifumo kama hiyo inazingatia Katiba hii.
46. HAKI ZA WATUMIAJI (CONSUMERS)
(1) Watumiaji wana haki ya-
(a) Kupata bidhaa na huduma za ubora wa kukubalika;
(b) Habari za kuwafaa kunufaishwa vilivyo na bidhaa na huduma hizo;
(c) Kulindwa afya yao, usalama wao, na maslahi yao ya kiuchumi; na
(d) Kufidiwa kwa hasara au matatizo yatayotokana na bidhaa au huduma hizo.
(2) Bunge litatunga sheria ya kuhakikisha ulinzi wa watumiaji na wa matangazo huru, kweli na ya kufaa (fair, honest and decent advertising).
(3) Kifungu hiki kinaangazia/ inatumika kwa bidhaa na huduma zitakazotolewa na mashirika ya umma au watu binafsi.
47. HATUA YA HAKI YA KIUTAWALA (FAIR ADMINISTRATIVE ACTION)
(1) Kila mtu ana haki ya kuwajibikiwa na utawala kwa haraka, ipasavyo kwa ufanisi, kisheria, reasonable na njia za usawa (expeditious, efficient, lawful, reasonable and procedurally fair).
(2) Ikiwa haki au huru za kimsingi za mtu zimeathiriwa au kuna hatari ya haki na huru hizo utatizwa kabisa na hatua ya kiutawala, mtu huyo ana haki ya kupewa sababu katika maandishi ya hatua hiyo.
(3) Bunge litatunga sheria ya kuidhinisha haki zilizotajwa katika Clause 1 na sheria hiyo -
(a) Itatoa nafasi ya kurekebishwa kwa hatua hiyo ya kiutawala na mahakama au, ikiwezekana mahakama huru maalumu na isiyoegemea upande wowote (independent and impartial tribunal); na
(b) Kukuza uongozi wa kufaa kwa ufanisi (promote efficient administration).
48. UWEZO WA KUPATA HAKI
Serikali itahakikisha uwezekano wa kupa haki kwa watu wote na malipo yoyote yakihitajika, yatakuwa ya kufaa na hayatazuia uwezekano wa kufanyiwa haki.
49. HAKI ZA WALIOKAMATWA (ARRESTED PERSONS)
(1) Mtu aliyekamatwa ana haki ya
(a) Kuelezwa unyo unyo, kwa lugha ambayo anaelewa:
(i) Sababu ya kukamatwa kwake
(ii) Haki ya kubaki kimya; na
(iii) Matokeo ya kutokimya
(b) Kubaki kimya
(c) Kuzungumza na wakili, au mtu mwingine ambaye usaidizi wake unahitajika
(d) Dhidi ya kulazimishwa kukiri au kukubali mashtaka, ambazo zinaweza tumika kama ushahidi dhidi ya mtu huyo
(e) Kuwekwa kando na wale ambao wamehukumiwa kifungo.
(f) Kuletwa mbele ya mahakama haraka iwezekanavyo, lakini sio baada ya
(i) Masaa ishirini nan ne baada ya kukamatwa
(ii) Ikiwa massa ishirini nan ne itaisha wakati ambao mahakama haijafunduliwa, au itaisha siku ambayo mahakama haijafunguliwa, ataletwa mahakama kabla ya mwisho wa siku ya kwanza ya mahakama kufunduliwa.
(g) Atakapokuja mbele ya mahakama kwa mara ya kwanza, anahaki ya kushtakiwa au kupwewa sababu ya kuendelea kuzuiliwa kwake, au kuwachiliwa; na
(h) Kuwachiliwa kwa dhamana aina ya bond au bail na kupewa masharti inayofaa, akingoja kushtakiwa au kuhukumiwa (pending a charge or trial) unless kuna sababu mwafaka ya kutowachiliwa kwake.
(2) Mtu hatazuliwa kwa kosa ambayo adhabu yake ni faini au kifungo chini ya miezi sita.
50. HAKI KATIKA KUSIKIZWA KWA KESI
(1) Kila mtu ana haki ya kutaka mzozo wowote unaoweza kusuluhishwa kwa kutumia sheria kuamuliwa katika kikao cha haki mbele ya mbele ya mahakama au, ikiwezekana shirika au mahakama maalumu iliyo huru na isiyoegemea upande wowote.
(2) Kila mshtakiwa ana haki ya kesi yake kusikizwa kwa njia ya haki, ikiwemo haki ya-
(a) Kuaminiwa kutokuwa na kosa hadi ithibitishwe kinyume;
(b) Kuarifiwa kuhusu mashtaka na taarifa ya kutosha kuyahusu kumwezesha kuyajibu;
(c) Kuwa na wakati na vifaa vya kutosha kutayarisha nyenzo za kujitetea;
(d) Kushtakiwa mbele ya mbele ya mahakama ya umma iliyowekwa na Katiba hii;
(e) Kuanzishiwa na kumaliziwa mashtaka bila kucheleweshwa;
(f) Kuwepo wanaposhtakiwa isipokuwa endapo tabia ya mshtakiwa inatatiza vikao vya mashtaka hayo;
(g) Kuchagua, na kuwakilishwa na wakili na kuelezwa kuhusu haki hii moja kwa moja;
(h) Kuwa na wakili aliyetolewa na Serikali kwa gharama ya Serikali yenyewe, endapo haki ya msingi itakosekana kwa kukosa wakili, na aarifiwe kuhusu haki hii moja kwa moja;
(i) Kunyamaza, na kutotoa ushahidi wakati wa vikao;
(j) Kuarifiwa mbeleni ya ushahidi ambayo upande wa mashtaka unanuia kutegemea, na kupewa reasonable access kwa ushahidi huo.
(k) Kuleta na kupinga ushahidi;
(l) Kutolazimishwa kutoa ushahidi wa kujifunga/kujishtaki;
(m) Kuwa na usaidizi wa mtafsiri bila ya kulipishwa endapo mshtakiwa hawezi kuelewa lugha inayotumiwa katika mashtaka;
(n) Kutohukumiwa kwa kitendo, au kosa ambalo wakati wa utendekaji au ukosaji halikuwa-
(i) Kosa nchini Kenya; au
(ii) Kosa la jinai chini ya sheria ya kimataifa;
(o) Kutoshtakiwa kwa kosa la kulinganishwa na tendo au kosa ambalo mtu huyo ashawahi achiliwa au kuhukumiwa kwalo;
(p) Kunufaika kwa angalau adhabu ndogo kabisa katika adhabu zilizoagizwa endapo adhabu iliyoagizwa kwa kosa lake imebadilishwa kati ya muda wa utendekaji wa tendo hilo na wakati wa kuhukumiwa; na
(q) Kukata rufani au kurejelewa kwa kesi hiyo na mahakama ya kiwango cha juu
(3) Kila mara Kifungu hiki kinataka taarifa kupeanwa, taarifa hiyo itatolewa katika lugha anayoelewa mtu huyo.
(4) Ushahidi unaopatikana katika njia inayokiuka haki yoyote au uhuru wowote wa kimsingi uliodokezwa katika Sheria ya Haki utawachwa endapo utekelezaji wa ushahidi huo utafanya mashtaka kukosa haki au uwe kizuizi katika utoaji haki.
(5) Mshtakiwa–
(a) Anayeshtakiwa kwa kosa fulani, kando na kosa ambalo mahakama inaweza kukamilisha kwa haraka, ana haki ya kupata nakala ya rekodi za vikao vya mashtaka endapo ataomba.
(b) Ana haki ya kupata nakala ya vikao vya mashtaka kwa wakati unaofaa baada ya kukamilishwa kwa vikao hivyo, kwa malipo fulani inavyoagizwa na sheria
(6) Mtu anayehukumiwa kwa kosa la jinai anaweza kulalamikia Mahakama Kuu ili kufanywe mashtaka mapya endapo-
(a) Rufani yake imetupiliwa mbali na mahakama ya ngazi za juu ambapo huyo mtu alikuwa na haki ya kukata rufani, au mtu ambaye hakukata rufaa kwa muda unaoruhusiwa kufanya hivyo, a
(b) Kutakuwa na ushahidi mpya na wa kukubalika/kushawishi.
(7) Kwa sababu ya kudumisha haki, mahakama inawezakubalisha mpatanishi kumsaidia mlalamishi au mshtakiwa kuweza kuwasiliana na mahakama.
(8) Hakuna chochote katika Kifungu hiki kitakachozuia kutengwa kwa wanahabari au raia wengine dhidi ya vikao vyote au vyovyote vya mahakama kwa sababu za kuwalinda mashahidi na wahusika wengine, maadili, amri ya umma au usalama wa kitaifa itakavyohitajika katika jamii huru na ya kidemokrasia.
(9) Bunge litatunga sheria kulinda haki na maslahi wa wahanga wa makossa.
51. HAKI ZA WALIO VIZUIZINI (DETAINED, HELD IN CUSTODY OR IMPRISONED)
(1) Mtu yeyote anayezuiliwa chini ya sheria, au kufungwa jela (detained, held in custody or imprisoned) anazo haki zote na uhuru wa kimsingi uliopo chini ya Katiba hii, isipokuwa endapo ni kwa ikwango kwamba haki au uhuru huo wa kimsingi hauambatani kabisa na sababu yake ya kuwa jela –
(2) Mtu yeyote aliye kizuizini atakuwa na haki ya kufukishwa mahakamani ili isikizwe kesi yake.
(3) Bunge litatunga sheria ambayo
(a) litatoa nafasi ya kushughulikiwa kibinadamu kwa walio kizuizini
(b) Inazingatia nyenzo mwafaka za haki za banadamu kimataifa.
SEHEMU YA TATU- UTUMIZI MAALUM YA HAKI
52. TAFSIRI YA SEHEMU HII
(1) Sehemu hii inafafanua baadhi ya haki ili kuhakikisha kupewa haki na huru hizo za kimsingi kwa makundi fulani ya watu
(2) Sehemu hii haitachuliwa kama kwamba inakatiza au kuzuia haki yoyote
53. WATOTO
(1) Kila mtoto ana haki-
(a) Jina na uraia kuanzia anapozaliwa na kusajiliwa kwa kuzaliwa kwao;
(b) Elimu ya bure na ya lazima;
(c) Chakula cha kutosha, makazi, huduma za malezi ya kiafya;
(d) kulindwa dhidi ya kunyanyaswa, neglect, tamaduni za kuumiza, aina zote za ukatili, kutumiwa vibaya,adhabu na matendo za kinyama na a kazi yoyote itakayohatarisha maslahi yao;
(e) malezi na kulindwa na wazazi wote, ambayo ni pamoja na jukumu ya ruzuku (provision) kutoka kwa mama na baba bila kuzingatia ikiwa wameoana au la; na
(f) ) Kutofungwa isipokuwa endapo hiyo ndio hatua yamwisho, na, wakishikwa au kufungwa, kufungwa
a. Kwa muda mfupi
b. kutenganishwa na watu wazima na washughulikiwe katika njia ambayo inazingatia umri na jinsia ya mtoto huyo-
(2) Maslahi bora ya mtoto ndio ya umuhimu mkuu na wa kuzingatiwa katika kila jambo linalohusu mtoto huyo.
54. WALEMAVU
(1) Mtu mwenye ulemavu wowote ana haki-
(a) Kuheshimiwa na kupewa maadili ya kibinadamu ikiwemo, kuzungumziwa na kurejelewa, katika njia na maneno yasiyowadunisha au kuwadhalilisha;
(b) Kuafikia elimu na taasisi na vifaa vya walemavu vilivyomo katika jamii na kwa jinsi inavyopaswa kutumiwa kwa maslahi yao
(c) Kuafikia ipasavyo sehemu zote zinazofikwa na umma, usafiri wa umma na habari na mawasiliano
(d) Kutumia lugha ya ishara, Breli na njia nyingine mwafaka za mawasiliano;
(e) Kuafikia nyenzo na vifaa vinavyoweza kuwasaidia kuukabili ulemavu huo; na
(2) Serikali itachukua hatua progressively ili kuhakikisha kuwa angalau asilimia tano ya waliochaguliwa katika vyoe elective and appointive ni watu wenye ulemavu.
55. VIJANA
Serikali itachukua hatua ikiwemo mipango ya usawa (affirmative action programmes) kuhakikisha kwamba vijana-
(a) Wanayo nafasi ya elimu na mafunzo inayofaa
(b) Wananafasi ya kushiriki, kuwakilishwa na kushiriki katika siasa, na maswala ya kijamii, kiuchumi na katika mawala mengine ya maisha;
(c) Kupata kazi; na
(d) Kulindwa vijana dhidi ya tamaduni zinazodhalilisha maadili na hadhi ya maisha yao.
56. MAKUNDI MADOGO NA MAKUNDI TENGWA
Serikali itachukua hatua za kisheria na nyinginezo kuweka mipango ya usawa iliopangwa kunufaisha makundi tengwa katika jamii kuhakikisha kwamba –
(a) Yanashiriki na kuwakilishwa kwa ukamilifu katika uongozi na katika anga zote za maisha;
(b) Yanapewa nafasi maalumu katoka nyanja za elimu na uchumi;
(c) Yanapewa nafasi maalumu ya kuafikia ajira ya kufaidisha
(d) Yanasaidiwa kukuza tamaduni zao, lugha na kaida zao;
(e) Yanasaidiwa kufikia maji, huduma za afya na infrastructure (miundombinu)
57. WAZEE KATIKA JAMII
Serikali itachukua hatua za kisheria na za kisera kuwahakikishia wazee haki za-
(a) Kushiriki kwa ukamilifu katika maswala ya jamii;
(b) Kufanya shughuli za maendeleo yao;
(c) Kuishi katika maadili na heshima na kuwa huru dhidi ya aina zote za ubaguzi na kutumiwa; kuhifadhi hadhi zao kijamii, kiuchumi na kisiasa; na
(d) Kupata malezi ya kufaa na usaidizi kutoka kwa familia zao na Serikali.
Endnotes....................... [1] The people does not translate to “Wakenya” as other translations have suggested, however it hardly lends itself to translation and the preference for Wakenya is appropriate. ‘Jumuia” is suggested or “Jumuia ya Kenya” [2] Wingi as opposed to Tofauti is chosen because of personal preference for translating diversity as a numerical concept rather as inherent difference. Tofauti carries a negative connotation in my view. [3] Utawala wa sheria preferred as opposed to utawala wa kisheria because in my view the latter lends itself as lawful rule as opposed to Rule of Law. The ki- denoted a manner of doing something rather than the thing itself. [4] Sovereign hardly lends itself to translation. “Kuu na kamilifu” is suggested because sovereignty in law has the connotation of dominance (kuu) and self-sustaining (kamilifu) [5] Inalienable also hardly lends itself to translation. Zisizoshindwa (inviolable/undefeated) is preferred because inalienable rights cannot be overridden by any justification and are deemed to withstand any challenge to the contrary. [6] Adopt does not directly lend itself to translation. Acceptance is the closest term that I could think of which translates to “kubali” [7] Usually when Parliament enacts a law it is termed as “kuipitisha’ which does not also directly translate to enact. [8] Jumuiya ya as opposed to raia wa because Raia has a citizenship and individual connotation while the people is a collective term and is more in line with the term Jumuia which is of communal connotation [9] The translation does not stay true to the original term. However, the Article is exclusive in nature and that aspect can only be translated through a change of phrase (True to substance). The translation “na zitatumika tu kulingana na katiba hii” is true to form. [10] Both Legal and Valid are translated as Halali in Swahili yet they are different concepts in legal terminology.Halali lends itself more to Legality. [11] Legal Validity is concerned with the enforceability of a rule by legal coercion. That it can be recognized. For this reason, utekelezaji is chosen because it implies that the constitution can be enforced. [12] Mapatano is the suggested translation for convention. Mkataba being Treaty [13] Access? Access to services? [14] Limejumuisha better translates into consists of rather than is divided into [15] Sharing? [16] Human dignity? [17] Equity and equality are not distinguished in Kiswahili. [18] supra [19] Presumed is not directly translatable to Swahili [20] Dual citizenship is a misnomer since there is nothing in the constitution that restricts, in my opinion, multiplicity of citizenship beyond 2 countries. It is therefore more of Multiple citizenship or Poly-citizenship. The translation in other documents was Uraia mara mbili. For the reasons given, I have given a different translation. [21] haki ya kuishi connotes Right to live which in my opinion is not equivalent to the right to life. Haki ya kuwa hai, is also not a proper translation.